Main Menu

Saturday, March 9, 2013

UHURU KENYATTA RAIS WA NNE WA JAMHURI WA KENYA BAADA YA KUMSHINDA RAILA ODINGA



Uhuru Kenyatta ndiye Rais wa nne wa Jamuhuri ya Kenya baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza kushinda uchaguzi wa kihistoria wa Kenya.

Ni baada ya siku tano tangu wakenya kupiga kura kuwachagua rais, magavana, maseneta , waakilishi wa bunge, waakislihi wanawake na waakilishi wa wodi.

Uhuru alipata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zilizohitajika ili kupata ushindi kulingana na mahitaji ya katiba mpya ya nchi.

Matokeo hayo yalionyesha kuwa Uhuru Kenyatta ameshinda na hivyo kuepuka duru ya pili ya uchaguzi.
Takwimu kutoka tume ya uchaguzi zinasema Kenyatta ameshinda asilimia hamsini nukta tatu za kura zote zilizopigwa.

Tume ya uchaguzi ilichukua zaidi ya masaa matano kukagua hesabu ya kura hizo kabla ya kutangaza matokeo hii leo siku tano baada yawakenya kupiga kura.

Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila Odinga akipata 5,340,546

Kenyatta anakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.

Awali duru zilisema iwapo Kenyatta atakabidhiwa ushindi katika raundi ya kwanza, mpinzani wake waziri Mkuu Raila Odinga atakwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.

Tume hiyo pia imemtangaza mshindi wa uchaguzi huo kwa kuwa ametimiza masharti ya kikatiba ya kutangazwa kuwa rais wa nne wa Kenya..

Vile vile mgombea huyo pia lazima awe ameshinda asilimia 25% katika nusu ya County zote 47 nchini kenya.
Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi na mipaka Isaka Hassan amemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa rais mpya wa Kenya.

Awali Waziri Mkuu Raila Odinga alikuwa amewaalika waandishi wa habari nyumbani kwake kwa mkutano maalum ili azungumzie maswala ya matokeo ya urais lakini baadaye mkutano huo uliakhirishwa, baada ya tume ya uchaguzi kutoa tangazo lake la mwisho.

Raila Odinga wa muungano wa CORD, ameelezea malalamishi kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta.

Odinga amesema kuwa udanganyifu ulitokea katika shughuli ya kuhesabu kura kwa kutumia mfumo wa zamani baada ya mitambo ya elektroniki kugoma hali iliyohujumu demokrasia.

Mseamaji wa Raila Odinga, Anyang' Nyong'o asema kuwa muungano wa CORD ulipinga matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa urais na kuitaka tume ya uchaguzi kutoyatangaza lakini walipuuzwa.

0 comments:

Post a Comment