Main Menu

Tuesday, January 15, 2013

WANANCHI WAKIMBIA MAKAZI YAO NCHINI MALI

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, makumi kwa maelfu ya raia wa kaskazini mwa Mali wameendelea kuyakimbia makazi yao wakihofia usalama wa maisha yao kutokana na operesheni ya kijeshi dhidi ya makundi ya waasi katika maeneo hayo. 

Eduardo Del Buey, Msemaji wa Umoja wa Mataifa amewaambia wana habari kwamba, inakadiriwa kwamba, raia elfu thelathini wameshayakimbia makazi yao kaskazini mwa Mali. 

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amebainisha kwamba, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Mauritania imethibitisha kuingia nchini humo maelfu ya wakimbizi wakitokea Mali. 

Vikosi vya Ufaransa ambavyo viko nchini Mali kwa ajili ya kuvisaidia vikosi vya serikali ya Bamako katika kupambana na makundi ya waasi ya kaskazini mwa nchi hiyo, jana vilifanya mashambulio makubwa ya anga katika ngome za waasi hao. 

Wakati huo huo imeelezwa kwamba, baadhi ya waasi wa kaskazini mwa Mali wamerejea nyuma kutoka katika maeneo wanayoyadhibiti kufuatia kushadidi mashambulio ya anga ya majeshi ya Ufaransa. 

Waasi hao wamesema kwamba, hatua hiyo ni mbinu ya kivita na sio kwamba, wamekimbia katika ngome zao.

CHANZO RADIO TEHRAN

0 comments:

Post a Comment