NEYMAR AGUNDULIKA KUWA NA UPUNGUFU WA CHEMBE HAI NYEKUNDU, MAN U YAITOSA OFA MPYA YA CHELSEA, UJERUMANI KATIKA KASHFA YA KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU MICHEZONI
Klabu
ya Barcelona inayoshiriki ligi kuu ya Hispania imebainisha mchezaji Neymar da
Silva anasumbuliwa na ugonjwa wa upungufu wa chembe hai nyekundu kwenye damu
kwa lugha kitaalamu Anemia.
Neymar
mwenye umri wa miaka 21 aligundulika ana tatizo la hilo wiki iliyopita wakati
wa vipimo vya afya. Anemia ni tatizo linalosababisha uchovu kwa kiasi kikubwa na
lina athiri maendeleo ya mchezaji.
Mkurugenzi
wa michezo wa timu ya Barcelona Andoni Zubizarreta alithibitisha kuwa Neymar
anasumbuliwa na tatizo hilo ingawa akasisitiza
mchezaji huyo anaendelea na matibabu chini ya jopo la matabibu wa klabu
hiyo.
Neymar
ambaye ni raia wa Brazil alijiunga na klabu ya Barcelona mwanzoni mwa mwezi wa sita
kwa ada ya Euro milioni 57 akitokea klabu ya Santos.
Klabu
ya Manchester united inayoshikiri ligi kuu ya England imekataa ofa ya pili ya
timu ya Chelsea ya paundi milioni 30 wakitaka kumsajili mshambuliaji Wayne
Rooney.
Manchester
united wameshikilia msimamo wa kutomuuza Rooney mwenye umri wa miaka 27 ambaye
anaonekana kupoteza furaha tangu mwishoni mwa msimu uliopita kutokana na
kutokuwa na uhakika wa namba kwenye kikosi cha kwanza.
Rooney
ambaye yupo ziarani nchini Sweeden na klabu yake ya Manchester united wakijiandaa na msimu mpya wa
ligi ameahidiwa kulipwa mshahara wa paundi laki mbili kwa juma kama atahamia
Chelsea .
Mtendaji
mkuu wa Manchester united Ed Woodward amesema pamoja na Rooney kubakisha
mkataba wa miaka miwili klabu hiyo haina mpango wa kumpa mkataba mpya
mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England.
Gwiji
wa zamani wa Uholanzi Johan Cruyff amesema nguvu ya pombe iliifanya wachezaji
timu ya taifa ya Ujerumani magharibi kufanya vizuri kwenye mashindano kombe la
dunia miaka ya 1960 mpaka 1970.
Cruyff
amesema anayohadithi juu ya madawa ya kuongeza nguvu kuwekwa kwenye
utayarishwaji wa pombe kitu kilichowasaidia wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani
magharibi kucheza kwa nguvu bila
kuchoka.
Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na chuo
kikuu cha Humboldt kilichopo Berlin kimegundua serikali ya Ujerumanini
magharibi ilikuwa ikichochea makampuni ya pombe kuweka madawa ya kuongeza nguvu
ili kuboresha afya za wanamichezo.
Cruyff
anakumbuka miaka ya zamani hakukuwa na upimwaji wa madawa ya kuongeza nguvu
michezoni kwasababu hiyo anafikiri ndio maana timu yao ya Uholanzi ilifungwa
kwenye fainali ya kombe la dunia na timu ya taifa ya Ujerumani magharibi mwaka
1974.
Na MVP Issa Maeda wa Ebony Fm
0 comments:
Post a Comment