Main Menu

Monday, July 22, 2013

MBASPO YA MBEYA NDIO MABINGWA KOMBE LA MUUNGANO MUFINDI 2013 YAIADHIBU MBEYA CITY


Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Angetile Osiah  akikabidhi kombe la  ubingwa  kwa  timu ya  Mbaspo  kutoka Mbeya  baada ya  kufanikiwa  kushindwa  kwa  mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya  wahasimu  wao Mbeya City katika faili ya kombe la Muungano Mufindi 2013 na kunyakua kombe na pesa kiasi cha Tsh milioni 3
 Mwenyekiti  wa chama cha  soka mkoa  wa Mbeya kushoto akiwa na mmoja kati ya  wachezaji wa  timu ya Mbaspo wakionyesha  kombe la ubingwa  leo katika  uwanja  wa  shule ya Msingi  Wambi mjini Mafinga.
 Mabingwa  wa mashindano ya  kombe la Muungano Mufindi mwaka 2013 timu ya Mbaspo ya Mbeya  katika  picha ya pamoja na mashabiki wageni  rasmi na  wadhamini   jioni ya leo katika  uwanja  wa Wambi mjini Mafinga.


Timu ya  Mbaspo kutoka mkoani  Mbeya  jana  imeibuka bingwa  wa mashindano ya kombe la Muungano  2013  baada ya  kuigagadua  kwa  jumla ya mikwaju ya  panelt 5-4 timu ya Mbeya  City  katika  mchezo  wa fainali  uliochezwa katika  uwanja wa  Shule ya  Msingi  Wambi mjini Mafinga  mchezo  ulioshuhudiwa na mgeni  rasmi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Angetile Osiah.

Katika mashindano  hayo mshindi  wa kwanza  timu ya  Mbaspo imekabidhiwa  pesa kiasi cha  Tsh milioni 3  Mendani na  kombe ,mshindi wa  pili Mbeya City  akinyakua mendani na Tsh milioni 1.5 wakati  mwamuzi  bora na mchezaji  bora  kila mmoja  akinyakua Tsh 400,000

Mratibu  wa mashindano  hayo Daud Yassin Amewapongeza  wadhamini  wa mashindano  hayo ikiwemo kampuni ASAS LTd ya  Iringa,kampuni ya Mwananchi Communication,NSSF,Pareto,Ibrahim Khamis, PPF,MUcoba Benk na  Chai Bora kwa  kufanikisha  mashindano  hayo.


Na Francis GodwinBlog


0 comments:

Post a Comment