Main Menu

Saturday, June 1, 2013

EBONY FM YATIMIZA MIAKA 7 YA KUTOA HUDUMA KUPITIA MASAFA YA FM NA ON LINE

   mafundi wakifunga vyombo vya bendi katika club la parte kwa ajili ya kusheherekea miaka saba ya ebony fm

    wageni kutoka tanapa wakiwa katika kipindi cha morning xtra asubuhi ya leo kutoka kulia ni godwell ole meing'ataki wa SPANEST na katikati risala kabongo wa tanapa, kushoto abdulfatah murtadha mtangazaji.





Kituo cha radio cha Ebony fm leo kimetimiza miaka 7 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006 mkoani iringa kikianza na masafa ya 87.8 pekee.

Kwa hakika kituo hicho kimechangia kwa kiasi kikubwa kusukuma maendeleo ya mikoa ya nyanda za juu kusini kwa stlye yao ya kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake kama redio imekua na mafanikio makubwa kwa upande wa urushaji matangazo kwa kuweza kuongeza masafa kutoka mkoa mmoja hadi mikoa mitano ya Iringa 87.8, Njombe 88.2, Mbeya 94.7, Morogoro 95.4, Dodoma 91.6, na Songea 102.2.

Pia redio hiyo imekua na mchango mkubwa katika utoaji elimu na burudani kwa kuendesha matamasha makubwa nyanda za juu kusini likiwa tamasha kubwa la Mtikisiko, Miss iringa na mengine mengi ikiwa ni pamoja na kumiliki club ambapo ivi karibuni wanatarajia kufungua club yao ya kisasa ijulikanayo kama La Parte.

Tofauti na miaka mingine ambapo kituo hicho kilikua kinaadhimisha kwa kuwashukuru wasikilizaji wake kwa kufanya tamasha lakini mwaka huu imekua tofauti kwa kuamua kuhamasisha wananchi kufanya usafi na kutunza mazingira katika maeneo yao.

Radio hiyo ipo chini ya Big Time Highlands Co Ltd

Namaliza kwa kusema HAPPY BIRTHDAY EBONY FM

0 comments:

Post a Comment