Main Menu

Thursday, April 30, 2015

NDANDA SC KUWAZA KULIPA DENI AU KUSHUKA DARAJA...?



WAKATI ikiwaza namna ya kujinasua na kushuka daraja, Klabu ya Ndanda SC imeamuriwa kumlipa mchezaji Amiri S. Msumi kiasi cha fedha sh. 2,600,000.

Pia Kamati ilihoji mkataba kutokuwa na kipengele cha mshahara, na kusema ni lazima mkataba uonyeshe Kiasi ambacho mwajiriwa analipwa.

Pia Kamati imeagiza kuwa vilabu vifahamishwe kuwa fedha ya kusaini mkataba (sign on fee) hazitakiwi kulipwa kwa mafungu. Tafsiri ya fedha ya kusaini, ni mchezaji kulipwa fedha yote baada ya kusaini, na si kwa mafungu.

Pamoja na uamuzi huo, Katibu Mkuu wa Ndanda SC ametakiwa kuwepo kwenye kikao cha Mei 3, 2015.

0 comments:

Post a Comment