Main Menu

Thursday, April 30, 2015

CHANONGO AONGEZA NJAA SIMBA, ATAKIWA KULIPWA MIL. 11



Wakati viongozi wa klabu ya soka ya Simba wakilalamika kushuka kwa mapato, Timu hiyo imetakiwa kuwalipa wachezaji iliyovunja nao mkataba na kuwatoa kwa mkopo.

Agizo hilo limetolewa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF likimhusisha mchezaji haruni chanongo .

Klabu hiyo inatakiwa kumlipa mchezaji Haruni Chanongo sh. 11,400,000,  kufikia Aprili 30, 2015 ambayo ni leo vinginevyo Sekretarieti ya TFF itaanza kukata mapato ya Simba ili kumlipa mchezaji huyo. 

Iwapo Simba itakuwa na vielelezo vingine katika kikao kinachofuata cha Kamati kitakachofanyika Mei 3, 2015 itafanywa hesabu na Simba kurejeshewa fedha itakayokuwa imezidi.

Kamati hiyo imeiagiza klabu ya Simba na klabu nyingine zote kuwa kwa wachezaji wa mkopo, maslahi yao (mishahara na posho) yote yalipwe na klabu husika kwa klabu ambayo mchezaji anakwenda kwa mkopo ili malipo yake yawe yanafanyika kutoka kwenye klabu moja badala ya kufuatilia malipo yake katika klabu mbili tofauti, hali ambayo inaweza msabababishia usumbufu mchezaji aliye kwenye mkopo.

0 comments:

Post a Comment