Main Menu

Thursday, April 30, 2015

AMISSI TAMBWE AONGEZA MACHUNGU SIMBA SPORTS CLUB




Mchezaji Amissi Tambwe aliwasilisha malalamiko dhidi ya Simba ya kutolipwa dola 7,000 za Marekani zilizotokana na klabu hiyo kuvunja mkataba wake Desemba 15, 2014.

Uamuzi wa kuvunja mkataba ulikuwa ni wa makubaliano ya pande zote ambapo Simba ilitakiwa iwe imemlipa fedha hizo mlalamikaji kufikia Desemba 17, 2014.

Katibu Mkuu wa Simba SC , Steven Ally alikiri klabu yake kudaiwa na mchezaji huyo na kuwa wameshafanya mawasiliano na wakili wake aliyepo Ureno, Felix Majani na kupanga utaratibu wa kulipa isipokuwa kinachosubiriwa ni kusaini hati ya makubaliano ya malipo (Deed of Settlement).

Kamati imesikitishwa na klabu ya Simba kushindwa kumlipa mchezaji huyo kama ilivyokuwa katika makubaliano ya kuvunja mkataba yaliyofikiwa na pande zote mbili Desemba 15, 2014.

Klabu ya Simba inatakiwa kumlipa Amissi Tambwe fedha hizo kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ya dola 5,000 malipo yawe yamefanyika kufikia Aprili 30, 2015. Salio la dola 2,000 ili kukamilisha jumla ya dola 7,000 liwe limelipwa kufikia Mei 10, 2015, uamuzi ambao upande wa Simba ulikubaliana nao.

0 comments:

Post a Comment